Kwenye zile headlines za 255 leo Witness amesema kundi la ‘Female Rappers’ walikutana ili kujifunza biashara kwa njia ya online kwani wengi wamekuwa wakifanya kimakosa, pia wamezungumzia suala la mavazi na wengi wao wamekubaliana kubadilika na kuvaa mavazi yenye heshima zaidi kama wanawake.
AT nae ana story nyingine leo, jamaa amesema sababu ya muziki wa Bongo Fleva kushindwa kutoboa Kimataifa ni kutokana na uelewa mdogo… anasema yeye anaufananisha muziki huo na nchi ambayuo haina Wimbo wa Taifa au nchi isiyo na bendera.
AT amesema muziki huo bado hauna utambulisho ndio sababu haufiki mbali.
Juma Nature ni staa wa Bongo Fleva, mastaa wengi tumeona wanapigia Kampeni Wagombea mbalimbali kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa TZ 2015, yeye vipi? Nature amesema yupo kibiashara zaidi kwenye kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu, yeye anachokifanya ni kuangalia upande gani unaweza kunufaisha Maisha yake, ikitokea akaitwa sehemu yoyote anaenda.
Stori zote nilizinasa kwenye 255 ya September 07 2015 kupitia #XXL ya @CloudsFM, ukiplay hapa utazisikiliza zote mtu wangu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos