Baada ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe anayeichezea club ya Dar es Salaam Young Africans Donald Ngoma, leo June 27 2017 zimeripotiwa taarifa za mchezaji huyo kujiunga na timu mpya.
Ngoma ambaye alikuwa akisumbuliwa na tatizo la goti na nyonga mara kwa mara akiwa Yanga, imeripotiwa na mtandao wa kickoff.com kuwa ameamua kujiunga na club ya Polokwane City FC ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mkataba wa Ngoma na Yanga unatajwa kuwa utamalizika mwishoni mwa mwezi June, hivyo ameamua kujiunga na Polokwane inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini na tayari amefanya na vipimo vya afya, Polokwane City msimu uliyoisha imemaliza ikiwa nafasi ya 6.
VIDEO: All Goals Taifa Stars vs Lesotho June 10 2017, Full Time 1-1