Kamati ya hadhi na haki za wachezaji leo Jumatano ya September 6 2017, imetangaza kuafiki makubaliano ya Simba na Yanga kuhusu mchezaji Pius Buswita ambaye alifungiwa kwa kusaini timu mbili.
Buswita aliingia matatizoni baada ya kusaini Simba mkataba wa awali na kuchukua Tsh milioni 10 na baadae akasaini Yanga, kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za usajili kwa mchezaji mmoja kusaini timu mbili na adhabu yake huwa ni kufungiwa mwaka mmoja.
Kamati ya hadhi za wachezaji imekubali kumfungulia Pius Buswita acheze Yanga lakini kwa sharti la kurudisha Tsh milioni 10 za Simba na Yanga kuilipia gharama ya tiketi ya Buswita aliyolipiwa na Simba.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0