Top Stories

GUMZO JINGINE LA MANJI: Ni kuhusu Udiwani Mbagala Kuu

on

Bado headlines za Mfanyabiashara Yusuf Manji zinaendelea kukamata kwenye mitandao mbalimbali ambapo mbali na headlines za kesi zake zinazoendelea Mahakamani leo September 6, 2017 ameingia tena kwenye headline baada ya kuvuliwa Udiwani.

Itakumbukwa kuwa Manji alishinda Udiwani katika Kata ya Mbagala Kuu katika Uchaguzi Mkuu wa 2017 lakini amevuliwa kutokana na kushindwa kufanya majukumu yake ya uwakilishi wa wananchi kwa miaka miwili mfululizo.

Mstahiki Meya wa Temeke Abdallah Jaffari Chaurembo amesema moja kati ya mapungufu yaliyopelekea Manji kunyang’anywa kiti hicho ni pamoja na kutohudhuria vikao vingi vya Kata na Baraza la Madiwani jambo linaloondoa sifa yake kuwa Diwani wa eneo hilo.

>>>”Kazi ya Diwani ni kuwasilisha Taarifa za Kata katika Baraza la Madiwani na hivyo wakazi wa Mbagala Kuu wamekosa uwakilishi, hivyo amevunja kanuni za Halmashauri na Sheria za Serikali za Mtaa.” – Mstahiki Meya Abdallah Chaurembo.

Uliiona hii? UKAWA TENA!! Wasusia Bunge kwa mara nyingine wenzao wapya wakiapishwa

Hii je? Ni kweli Lissu kaalikwa kwenye mkutano wa wanasheria Duniani?

Soma na hizi

Tupia Comments