Staa wa zamani wa ManUnited na timu ya taifa ya Ufaransa ambaye anaichezea Marseille ya Ufaransa Patrice Evra ameguswa na kusikitishwa na matukio ya kigaidi yanayotokea mara kwa mara katika miji tofauti hususani lililotokea August 16 2017 jijini Barcelona na kuua watu 13 na zaidi ya majeruhi 100.
“Nimechoka kuona tuwaombee Barcelona sijui tuombee mji fulani kwa sasa imekuwa kawaida, watu wasiokuwa na hatia wanakufa, nipe sababu ya kumuua mtu fulani lakini naamini katika Mungu na hawa watu watapata hukumu ya mwisho”
“Mimi ni mchezaji soka, sio mwanasiasa sio Rais hivyo siwezi kuhukumu chochote lakini tunatakiwa kutafuta ufumbuzi wa kuondoa mauaji, huu sio muda wa kuishi kwa hofu, huu sio muda wa kuishi kwa chuki kwa sababu najua watu watakachosema kwa sasa kuwa ni waislamu waliyofanya hivi”
“Hujui chochote kuhusu hii dini, uislamu ni dini nzuri kwa sasa ni muda wa kufanya maombi na kusaidia familia ambazo zinapoteza watu zinaowapenda Nawaomba naomba acheni kuuwa watu bila sababu”
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Patrice Evra aliwahi kuichezea club ya Man United katika kipindi cha miaka nane, alianza kuichezea Man United mwaka 2006 baada ya kujiunga nayo akitokea Monaco, 2014 akaamua kujiunga na Juventus ya Italia kabla ya 2017 kuamua kujiunga na Marseille ya kwao Ufaransa.
“Nimechoka kuona sijui tuwaombee Barcelona, tuwaombee mji fulani kwa sasa imekuwa kawaida watu wasio kuwa na hatia wanakufa”-Patrice Evra pic.twitter.com/C6pvlrGa6G
— millard ayo (@millardayo) August 19, 2017
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0