Mwaka 2017 umemalizika na kila mtu tumeona akibaki na kumbukumbu zake nzuri na mbaya kwa mwaka 2017, wapo baadhi ya watu maarufu waliyoamua kuweka hadharani kumbukumbu zao nzuri na mbaya zilizowatokea kwa mwaka 2017, afisa habari wa Simba Haji Manara ni mmoja kati ya watu ambao wameamua kuweka wazi kumbukumbu zao 2017.
Salaam za mwaka mpya toka kwa Haji S Manara Msemaji wa Simba SC
Awali ya yote tumshukuru sana Mungu mwenyezi kwa kutuwezesha sote kuumaliza mwaka 2017 na kuuingia mwaka huu mpya wa 2018, mwaka tulioumaliza ulikuwa na changamoto nyingi sana kama ilivyo kwa miaka yote ya nyuma, Changamoto tulizopitia ni za kawaida sana ingawa nyingine zilikuwa ngumu sana, kiasi cha kwamba zimeacha doa kwenye maisha yetu.
Mojawapo ya changamoto iliyonigusa sana mwaka jana, ni kushtakiwa kwa viongozi wakuu wa klabu nnayoisemea ya Simba. Kufunguliwa kwa Shauri lile sio tu kulinihuzunisha, bali kulinifanya niwe muoga sana kwa kila kitu. ila kama nilivyoandika ni changamoto tu na mwanadamu huna budi kupitia mitihani ya aina hii ili kukamilisha ubinadamu wako, sote tumuombe Mungu aiwezeshe kesi hii iishe haraka na haki ipatikane kwa pande zote.
Mwaka jana pia kama klabu na kama Timu tulipata changamoto kubwa ya vyombo vyenye maamuzi ya kuongoza Soka nchini, kutoitendea haki klabu yetu kwa mambo kadha wa kadha, sio nia yangu kufukua makaburi, lakini lazma tujikumbushe ile kadhia tata ya kadi tatu za njano, ambayo kwa makusudi kabisa waliokuwa viongozi wa TFF waliamua kulipindisha jambo lile ili tu waliepanga awe bingwa kupata walichopanga.
Haiwezekani na nitaendelea kuamini kamati iliyofanya maamuzi ya kuipoka Simba points tatu, haikuwa na mamlaka yoyote ya kutolea maamuzi ya jambo lililotokea uwanjani, Sote tunajua kila shauri hutolewa uamuzi na chombo ‘Makhsuus’.
Itakuwa ajabu ya karne eti Mahakama ya Ardhi kutolea maamuzi kesi za ubakaji, au kamati ya Bunge ya maadili kutolea uamuzi kesi za Trafiki, ni kituko kikubwa kuwahi kutokea nchini…. kwangu ulikuwa uonevu mkubwa zaidi kuwahi kutokea nchini, Lakini yalishaisha na sisi kama klabu tuliamua kusonga mbele zaidi.
Ni kweli Simba iliamua kulalamika FIFA baada ya kuona hatutapata haki kwa TFF ile, lakini chombo hicho kikubwa zaidi duniani kilitujibu kwa njia ya DHL,ya kwamba tutumie vyombo vya ndani kwenye Shirikisho na ushauri wao kwetu pia ulilenga kuzingatia muda wa malalamiko yetu.
Busara ya uongozi wa Simba chini ya kaimu Rais wa Simba Salum Abdallah kwenye jambo hili ilikuwa kubwa sana, kwa kuwa majibu ya FIFA
Juma Mahadhi alipopiga magoti kuomba msamaha Yanga
https://youtu.be/1oNJmyXQDfo