Leo May 5 2016 shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza rasmi kuwa klabu ya Azam FC imenyang’anywa point tatu na magoli matatu kutokana na kumtumia Erasto Nyoni ambaye alikuwa na kadi tatu za njano, katika mchezo wa 156 wa Ligi Kuu uliokuwa unazihusisha timu za Azam FC dhidi ya Mbeya City.
Baada ya taarifa hizo kutoka Sports Extra ya Clouds FM ilizungumza na afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC Saad Kawemba na kueleza “Kwa sasa tumewapatia hilo suala benchi la ufundi ili waweze kufuatilia na kuona uhalisia wa hicho kinachozungumzwa halafu watatueleza kama ni kweli kosa hilo limefanyika halafu tutajua nini cha kufanya”
Maamuzi ya TFF kuinyang’anya point tatu na magoli matatu Azam FC yanatokana na Kanuni ya 37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0