Hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea usiku wa Jumanne ya February 21 2017 kwa michezo miwili kuchezwa, mchezo wa Man City katika uwanja wao wa Etihad dhidi ya Monaco ya Ufaransa ulikuwa ni miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku huo.
Man City wameifunga Monaco goli 5-3 katika mchezo huo wa kwanza kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo, Monaco imekuwa miongoni mwa timu zilizokubali kipigo kikubwa katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya 16 bora baada ya Arsenal kukubali kipigo cha 5-1 kutoka FC Bayern Munich.
Licha ya Monaco kupoteza mchezo huo kwa idadi ya goli 5-3, wanarejea kwao Ufaransa wakiwa wameweka rekodi hadi sasa ndio timu pekee katika Ligi tano kubwa barani Ulaya iliyofunga magoli mengi zaidi kwa mashindano yote ndani ya msimu wa 2016/2017.
Monaco wanawapiku FC Barcelona kwa kufikisha jumla ya goli 111 huku FC Barcelona wakibaki nafasi ya pili kwa kuwa na goli 109, hii ni game ya 41 kwa Monaco ndani ya msimu huu huku mshambuliaji wao Radamel Falcao akifikisha jumla ya goli 24 msimu huu kwa kucheza jumla ya game 29.
https://youtu.be/rjdVR1Tsl2Y
Matokeo ya mechi za hatua ya 16 bora za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa February 21 2017. pic.twitter.com/xPmQTA9Kki
— millard ayo (@millardayo) February 21, 2017
FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5