Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo Ijumaa ya December 8 2017 limetangazaa maamuzi yaliowashitua mashabiki wengi nchini Peru, FIFA leo imetangaza kumfungia mwaka mmoja kucheza soka nahodha wa timu ya taifa ya Peru Paolo Guerrero.
FIFA imemfungia nahodha wa timu ya taifa ya Peru Paolo Guerro anayeichezea club ya Flamengo ya Brazil kutokana na kugundulika kutumia dawa ambazo kisheria za michezo haziruhusiwi kutumiwa na wanamichezo.
Adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja kwa Paolo Guerrero imeleta masikitiko makubwa nchini Peru hasa kwa kipindi hiki ambacho Peru wamefuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza toka 1982, Paolo watamkosa wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2018 Urusi.
Paolo Guerrero ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Peru amegundulika kuwa alitumia cocaine wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Argentina game ambayo ilimalizika kwa sare tasa 0-0.
VIDEO: Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja