Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa club ya Simba Haji Manara leo Jumamosi ya August 19 2017 alipata nafasi ya kuwa mgeni katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV na hoja kubwa ambayo alitakiwa kuijibu ni kueleza kwa kina mfumo mpya wa mabadiliko unaoendelea kwa sasa.
Kuna baadhi ya watu wanaotaka mabadiliko na kuna kundi jingine halitaki mabadiliko likiamini mfumo huo unalenga kumkabidhi timu mtu mmoja ambaye ni mfanyabiashara na bilione wa 16 wa Afrika Mohammed Dewji, Haji Manara amejibu hoja na kufafanua kuhusu mfumo huo.
“Club ya Simba baada ya valuation iliyofanyika ya kina watu wanasema valuation ya Simba ni zaidi ya Bilioni saba, brother mimi nimezaliwa Kariakoo najua thamani ya majengo, pale tuna majengo mawili, hata umlete yoyote aje kutathimini thamani haiwezi vuka zaidi ya bilioni tatu”>>> Manara
“Tuna kiwanja cha Bunju ambacho hakina muendelezo cha Bunju na vile vigari gari vyetu, weka na Brand juu maana watu wanasema Brand Brand lazima ifanane na uhalisia, kwa maana ya umaarufu Simba ndio taasisi maarufu kuliko taasisi zote ikiwemo nyinyi Clouds”>>>Manara
Afisa habari wa Simba SC Haji Manara akizungumzia mfumo mpya wa mabadiliko wa Simba leo #Clouds360 #Updates1 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/PmWmEchGyH
— millard ayo (@millardayo) August 19, 2017
Afisa habari wa Simba SC Haji Manara akizungumzia mfumo mpya wa mabadiliko wa Simba leo #Clouds360 #Updates2 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/lMt24WaLPH
— millard ayo (@millardayo) August 19, 2017
VIDEO: Ushindi wa Simba vs Rayon Sports, Simba Day 8 2017 Full Time 1-0