Staa wa Azam FC na nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Himid Mao leo September 5 2017 anatimiza miaka miwili mfululizo akiichezea Taifa Stars toka aichezee September 5 2015 katika mchezo dhidi ya Nigeria uliyomalizika kwa sare 0-0.
Toka September 5 2015 Himid Mao hajawahi kukosekana katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kila kinapoitwa, kwa miaka miwili mfululizo amekuwa akiitwa mara zote Taifa Stars, Himid Mao ambaye ni baba wa mtoto mmoja wa kike Balqees na ana mke, toka September 5 2015 hadi leo anakuwa kaichezea Taifa Stars jumla ya game 28.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0