Ni segment ambayo itakua na maisha marefu kwenye millardayo.com manake kila siku watu wanafikiria kujenga au kurekebisha nyumba zao na hii inasaidia kukusafishia Idea yako kwenye kila unachokitaka au bora zaidi yake.
Kwasababu mimi napenda sana kufatilia mambo ya nyumba, nimegundua nyumba nyingi za kizungu ninazoziona ziko simple sana yani hawana vitu vingi kwenye Sebule zao mpaka chumbani.
Kingine kikubwa ambacho nimekigundua ni kwamba wenzetu wanatumia sana sakafu za mbao sasa hivi kuliko tiles tulizozizoea…. sakafu za mbao hazihitaji kudekiwa bali kufutwa tu na dekio lenye unyevunyevu ili kuondoa vumbi.
Zamani muonekano wa nyumba kwa nje ulikua unaachwa sana hukohuko nje lakini siku hizi idea ya kuhamishia muonekano wa nje na kuuweka ndani ndio imebamba….. tazama walivyotumia vizuri matofali ya kuchoma hapa chumbani.
Kitu kingine nilichowanyanyulia mikono ni mgangilio na aina ya taa zinazotumika, nyumba lazima ivutie….
Wakati mwingine hawatumii matofali ya kuchoma kama inavyoonekana, kwenye maduka mbalimbali ya ujenzi kuna tiles zenye muonekano kama matofali ya kuchoma ambazo ukishazinunua unazibandika ukutani kwa kutumia Cement.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE