June 21 2016 jina la nahodha wa timu ya taifa ya Sweden aliyekuwa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Sweden baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika.
Zlatan amefikia maamuzi hayo ikiwa ni siku chache zimepita toka atangazwe katika list ya wachezaji wa Sweden watakaoicheza michuano ya Olympic Brazil, hizi zinatajwa kuwa ni habari njema wa Man United ambao wanatajwa kuwa watamsajili baada ya Euro, kwani atakuwa huru na muda mwingi zaidi wa kuitumikia klabu yao.
Nahodha huyo wa Sweden ameanza kucheza timu ya taifa toka 1999 akiwa timu za vijana na mwaka 2001 ndio alianza kucheza timu ya wakubwa “Mechi hizi za Euro 2016 ndio zitakuwa za mwisho mimi kuichezea Sweden, ni heshima kuwa nahodha wa Sweden kwa kipindi chote, popote nitakapoenda nitakuwa na bendera ya Sweden kwa sababu mimi ni msweden”
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE