CEO wa makampuni ya Quality Groups Limited Nicholaos Ralph leo March 15 2017 aliongea na vyombo vya habari na kueleza mambo mbalimbili kuhusu mipango ya kampuni yao katika kushirikiana na serikali na kuleta maendeleo Tanzania.
Ralph ambaye ndiye CEO wa makampuni za Quality Groups yanayomilikiwa na mfanyabiashara Yusuph Manji, ameeleza dhamira ya makampuni yao katika kuunga mkono na kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.
“Sisi kama Quality Groups tunaamini nchi yetu na Afrika kwa ujumla na tunaamini pia suluhisho la ndani katika matatizo ya ndani, tunaunga mkono mpango wa maendeleo wa Tanzania wa 2020/2025 na kuhakikisha kama sekta binafsi tunashirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.”
“Kama ambavyo mjuavyo wengi wenu kampuni ya Quality Group imekuwa ikijihusisha katika biashara mbalimbali za kilimo, viwanda na tunaendelea kuhakikisha tunafanikiwa katika upande huo licha ya kuwa serikali imekuwa ikizipa changamoto sekta binafsi na kutengeneza fursa mpya.”
AyoTV MAGAZETI: Undani kutimuliwa Sophia Simba, Madabida, Wapinzani na kauli za Magufuli