Leo January 16 2018 kupitia ukurasa wa instagram wa msanii Nikki wa Pili ambaye ni moja kati ya wasanii wa hiphop wanaounda kampuni ya Weusi, ameamua kugusia kile ambacho inaaminika kinahusiana na agizo la rais JPM akiwataka wasanii kuzingatia mavazi hasahsa kwenye music videos zao.
Nikki wa Pili ameandika
“Maoni yangu juu ya wasanii na maadili kidogo na tizama katika upana ni hivi .Kama tulivyo acha miiko ya uongozi, kama mwanasiasa anavyo nunuliwa au kuuza kura, kama dini ilivyo kuwa dili”
“Kama vyuo vinavyo fuata mahitaji ya soko, kama jamii inavyo tukuza mafanikio ya pesa bila kujali mtu anazipataje, Kama wachimbaji wadogo walivyo fukiwa wazima na maeneo yao kupewa mwekezaji”
“Basi ndivyo hivyo wasanii nao wamepoteza kufikiri juu ya maadili ya mavazi na tungo .Ni mfumo mzima wa kijamii tulio uchaguwa toka 1984 kwa neno ruska? Kama tuna hoji maadili ya wasanii je?? Maadili ya demokrasia ni yapi? Maadili ya uchumi ni yapi? Maadili ya elimu ni yap? Maadili ya siasa ni yapi? Maadili ya media ni kulinda maslahi yapi?”
MAADILI SWALI LA MSINGI TUJIULIZE????
Tale amwambia Ruby…. “Siku ukijua unaumwa nini……..”