Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ni moja kati ya watanzania waliyopokea kwa mshituko taarifa za mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu kupigwa risasi.
Tumeona watu mbalimbali wakioneshwa kufuguswa na tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa Tundu Lissu akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D Dodoma baada ya kurudi kupata chakula cha mchana akitokea Bungeni.
Baada ya Rais Magufuli kuzipata taarifa hizo za kushambuliwa kwa kupigwa risasi kwa Tundu Lissu alitumia ukurasa wake wa twitter kuonesha hisia zake alivyoguswa na tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu.
“Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka, Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria”>>> Rais Magufuli
VIDEO: Mbowe aeleze Tundu Lissu alivyoshambuliwa kwa risasi