Baada ya timu ya Taifa ya Sweden kufuzu kucheza michuano ya kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa kuitoa Italia ambayo imekuwa imara na rekodi nzito katika michuano hiyo kwa kufanikiwa kushiriki michuano kwa miaka 59 mfululizo toka 1958, Ibrahimovic kaongea
Sweden wanafuzu kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki fainali hizo kwa mara ya mwisho mwaka 2006 hivyo kufuzu kwa michuano hiyo kunaweza kumrudisha staa wa Man United Zlatan Ibrahimovic ambae alistaafu kuichezea timu ya taifa ya Sweden.
Zlatan Ibrahimovic baada ya kuona taifa lake limefuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Italia na nahodha wa Italia Gianluigi Buffon akilia kwa uchungu kwa kutolewa katika michuano hiyo, alipohojiwa Zlatan amenukuliwa akisema yafuatayo
“Buffon anaweza kulia kadri awezavyo lakini ukweli ni kuwa Sweden walistahili kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2018 hivyo anapaswa kukubaliana na hilo”>>> Zlatan Ibrahimovic
Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji