AyoTV

VIDEO: Justice Majabvi kaeleza sababu iliyomfanya aondoke Simba SC

on

Kwa mara ya kwanza katika exclusive interview AyoTV imempata kiungo wa zamani wa Simba Mzimbabwe Justice Majabvi, Majabvi alicheza Simba kwa msimu mmoja na katika msimu mmoja alicheza kwa asilimia 90 ya  mechi zote za Simba akionesha kiwango kizuri.

Baadae mwisho wa msimu alivyoenda kwao Zimbabwe hakutaka tena kurudi Simba, AyoTV imempata akiwa kwao Harare Zimbabwe nini kilimfanya aondoke Simba licha ya kucheza kiwango kizuri.

“Kwanza nilitaka kurudi nyumbani kukaa karibu na familia yangu na kuna vitu baadhi vilikuwa haviendi sawa kati yangu na timu, sasa sikutaka kumsumbua mtu wala ku make stori nikaona njia sahihi ni mimi kuondoka tu”

“Kama wanataka nirudi nilazima wazingatie professionalism unajua mimi ni mchezaji professional sitokei mtaani, katika maisha yangu ya soka sikuwahi kuwa na ugomvi na yeyote katika soka na sipendi migogoro, mimi napenda kucheza soka”

“Kwa sasa nipo tu sichezi mashindano yoyote zaidi naenda kucheza timu za malegend pale ninapojisikia haiko serious kihivyo, huwa najumuika na wachezaji wa timu za zamani, bado najihisi naweza kucheza na kufanya vizuri lakini ili nirudi kucheza ni lazima nipate mahali sahihi”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments