Baada ya headlines na shauku ya mashabiki wengi kutaka kushuhudia game ya Simba na Azam FC nani atakuwa mbabe, hatimae leo Jumatano ya February 7 2018 game hiyo imechezwa na mbabe amejulikana.
Game ya Simba dhidi ya Azam FC leo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu hizo zote hizo kufukuzana kwa karibu hivyo matokeo ya mchezo huo yalikuwa yanatarajiwa kuleta taswira mpya katika msimamo wa Ligi, hivyo kupoteza Azam FC kwa goli 1-0 kumeanza kuikatisha tamaa Azam FC katika mbio za Ubingwa kwa kuachwa point nane.
Kabla ya game ya leo Simba alikuwa kaizidi Azam FC kwa point 5, Azam wakiwa na point 33 na Simba 38, hivyo ushindi wa Simba wa goli 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 37 kipindi cha kwanza unaifanya Simba kujikita kileleni kwa tofauti ya point nane dhidi ya Azam na tofauti ya point 7 dhidi ya Yanga anayeshika nafasi ya pili.
Ushindi wa leo wa Simba dhidi ya Azam FC unakuwa ni ushindi wa Simba wa kwanza katika Ligi toka September 17 2016 Simba ilipoifunga Azam FC goli 1-0 lililokuwa limefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 67 ya mchezo uliyochezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, ambapo ni sawa na mwaka mmoja na siku 144 toka Simba aifunge Azam FC kwa mara ya mwisho katika Ligi.
VIDEOMagoli: Ushindi wa 4-0 wa Yanga vs Njombe Mji, Obrey Chirwa akipiga hat-tric