Winga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva leo asubuhi ya August 31 amewasili Dar es Salaam akitokea Morocco kwa ajili ya kuungana na Taifa Stars.
Msuva amewasili Tanzania ili kuungana na kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mchezo ambao upo kweye kalenda ya FIFA vs Botswana Jumamosi September 2 uwanja wa Uhuru ambapo hii ni mara ya kwanza kwa Msuva kurudi Tanzania toka ajiunge na Difaa El Jadid ya Morocco.
“Kwanza namshukuru Mungu kupata nafasi ya kucheza Morocco ni kweli napata tabu ya changamoto ya lugha kule wanazungumza kiarabu na kifaransa, mimi sijui kifaransa sijui kiarabu lakini naamini lugha ya mpira ni moja nitajifunza pale pale”
“Kuna changamoto ya chakula kuna vyakula nimekutana navyo huku nilikuwa naringa kula lakini kule natakiwa nivile maana wenye ndio wanasema vizuri kwa wachezaji na miss vyakula vya nyumbani kama wali unajua wali wa kule na huku tofauti lakini pia kule hakuna ugali” – Msuva
“Nikiwa Morocco na Difaa El Jadid nimecheza hadi sasa mechi 11 za kirafiki nimeshinda magoli tisa lakini nimekosa mechi moja ya King Cup maana ITC yangu ilikuwa haijafika lakini ya marudiano nimecheza na kufunga goli la tatu” – Msuva
Mtazame zaidi kwenye hii video hapa chini…..
Samatta kaipata ofa ya kumrithi Van Persie? ukimuuliza atakujibu hivi
HAUTAKI KUPITWA??? Kuna hii APP MPYA YA MILLARD AYO kwa wewe wa ANDROID unaweza kubonyeza hapa moja kwa moja kwenda kui-download mtu wangu, HABARI ZOTE KIGANJANI MWAKO >>> APP MPYA BONYEZA HAPA