July 1 2016 klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba imetangaza rasmi kuingia mkataba wa miaka miwili na kocha raia wa Cameroon Joseph Omog ambaye pia siku hiyo hiyo ya July 1 wamemtambulisha mbele ya waandishi wa habari.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Joseph Omog mwenye umri wa miaka 44 amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili, lakini ndio kocha aliyeipa Ubingwa Azam FC kwa mara ya kwanza katika msimu wa 2013/2014.
Hata hivyo Simba walitumia nafasi hiyo kumtambulisha rasmi katibu wao mkuu Patrick Kahemele, ambapo kwa mujibu wa mkataba wake leo July 1 2016 ndio atakuwa ameanza kazi rasmi.
Simba iliposaini mkataba wa miaka miwili na kocha Mcameroon Omog ambaye amewahi kuifundisha Azam FC na kuipa Ubingwa pic.twitter.com/1Me0ZZWWJM
— millard ayo (@millardayo) July 1, 2016
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE