Usiku wa June 17 2016 Mabingwa watetezi wa Kombe la Euro timu ya taifa ya Hispania, walikuwa na harakati za kuendelea kutetea taji lake dhidi ya timu ya taifa ya Uturuki katika mchezo wa pili wa Kundi D linaloongozwa na Hispania kwa jumla ya point 6.
Mchezo umemalizika kwa Hispania kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Uturuki ambayo kufutia kipigo hiko inakuwa imeaga rasmi michuano hiyo kutokana na kutokuwa na point hata moja, point tatu za Hispania zilipatika kwa magoli ya Alvaro Morata dakika ya 35 na 48 na Manuel Nolito dakika ya 37.
Andre Iniesta alifanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, hii ni mechi tatu mfululizo Uturuki inafungwa na Hispania, mechi mbili za mwisho kucheza, Hispania aliifunga Uturuki goli 2-1 April 1 2009 na goli 1-0 March 28 2009, Uturuki inakuwa timu ya tatu kuaga michuano ya Euro 2016 baada ya Albania na Ukraine.
Video ya magoli ya Hispania
https://youtu.be/f182mOeU6jg
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE