Baada ya usiku wa May 10 kufahamu fainali ya UEFA Champions League itazikutanisha timu gani, usiku wa May 11 2017 ndio ilichezwa michezo ya marudiano ya nusu fainali ya UEFA Europa League, Man United wakicheza dhidi ya Celta Vigo na Lyon wakicheza dhidi ya Ajax.
Game ya Man United ilimalizika kwa sare ya kufungana 1-1 goli la Man United likifungwa na Fellaini dakika ya 17 na goli la Celta Vigo lilifungwa dakika ya 85 na Roncaglio, sare hiyo imeiwezesha Man United kuingia hatua ya fainali baada ya mchezo wa kwanza kuifunga Celta Vigo goli 1-0 ugenini.
Ajax wao wamepoteza kwa magoli 3-1 lakini wamefuzu kuingia fainali kwa aggregate ya 4-5, Man United anafuzu kucheza fainali ya Europa League kwa mara ya kwanza wakati Ajax anafuzu kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 mara ya mwisho ilikuwa 1996.
Mchezo wa fainali ya UEFA Europa League itachezwa katika uwanja wa Friends mjini Stockholm nchini Sweden May 23 2017, hii inakuwa ni mara ya pili kwa kocha wa Man United Jose Mourinho kufanikiwa kufikia hatua ya fainali ya michuano hiyo akiwa na timu mpya katika msimu wa kwanza, mara ya kwanza ilikuwa 2002/03 akiwa na FC Porto ya kwao Ureno.
https://youtu.be/bFSsHzeTIFw
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera