Leo October 28 2016 hatimae majadiliano yaliodumu kwa siku takribani tatu yakisimamiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba, yamezaa matunda baada ya kocha Hans kuombwa abadili msimamo wake na arudi kazini kama kawaida, waziri Mwigulu ameeleza pia sababu na takwimu zilizomfanya ashawishi uongozi kumuomba kocha Hans van Pluijm arudi.
“Mimi nilichozingatia hadi kushawishi uongozi kumuomba kocha Hans van Pluijm arudi mimi kama mdau wa Yanga na mwanamichezo niliona timu ipo kwenye mashindano, lakini ina takwimu nzuri tangu mwalimu amekuja timu imechukua Ubingwa mara mbili mfululizo, tangu aje mwaka jana timu ilishinda vikombe vyote kuanzia Ngao ya Hisani”
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0