Shirikisho la soka Tanzania TFF leo November 22 2016 kupitia kwa kamati ya saa 72 imetangaza adhabu kadhaa kwa vilabu vya Ligi Kuu ikiwemo kumuadhibu kocha mkuu wa Yanga Hans van Pluijm kwa tuhuma za kuwatolea lugha chafu waamuzi wa mechi.
Kamati ya saa 72 imemfungia kocha Hans van Pluijm mechi tatu kukaa katika benchi na kumpiga faini ya Tsh 500,000 kwa kosa hilo, Hans anatajwa kuwatolewa lugha chafu waamuzi wakati wa mchezo na baada ya mchezo kuwafuata katika vyumba vya kubadilishia nguo.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas ametoa list ya vilabu na makocha waliopewa adhabu kutoka kamati ya saa 72 “Mechi namba 104 iliyowakutanisha JKT Ruvu na Ndanda, Ndanda imepewa onyo kali baada ya wachezaji wake kufanya vurugu kwa kutaka kuingia uwanjani bila kufanyiwa ukaguzi, kocha wa Azam amefungiwa mechi tatu na faini ya Tsh 500,000”
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0