AyoTV

VIDEO: Sababu za wafanyabiashara wa Zimbabwe kununua bidhaa Tanzania na sio Afrika Kusini

on

Najua umesikia headlines za taifa la Zimbabwe kuwa wanatumia dola ya Marekani kama ndio hela yao kutokana na noti yao kuanguka na sasa wapo katika mpango wa kutengeneza bond noti ili kukidhi uhaba wa dola nchini humo.

AyoTV ilikuwa Zimbabwe wiki kadhaa nyuma na kupita mitaa tofauti tofauti ya soko mjini Harare ikiwemo kwa wafanyabiashara wadogowadogo kwa Tanzania wanajulikana kama wamachinga, tumempata Ben ambaye ni mfanyabiashara wa viatu Zimbabwe ameeleza sababu ya bidhaa kuwa juu Zimbabwe.

dsc_5823

Ben

“Sababu ni rahisi unajua tunatoa hizi bidhaa Tanzania Kariakoo ambapo ni bei rahisi sana na kwa nini tunatumia Tanzania na sio Afrika Kusini ambapo ni Karibu na Zimbabwe ni kwa sababu Afrika Kusini bidhaa hizi za viatu sio original kwa asilimia 100 hivyo Afrika Kusini haziruhusiwi kuingia kutokana na kuwa pale kuna maduka kabisa ya viatu vya Nike, Reebok na Adidas Original kutoka America”

“ukisema uingize viatu aina hii original kutokea Afrika Kusini utashindwa kuviuza kwa sababu ya bei sasa ukisema utoe gharama zako za kuleta mzigo na kuuza huwezi kupata faida, hivyo viatu hivi haviruhusiwi Afrika Kusini kama ambavyo gari za kijapan haziruhusiwi”

VIDEO; RC Makonda alipofika kwenye soko la Stereo Temeke Dar es salaam

Soma na hizi

Tupia Comments