Club ya Yanga SC leo kwa kushirikiana na UNICEF wametangaza kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain utakaochezwa November 02, 2022 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa watatoa elimu ya kuchanja kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19 pamoja na kutoa elimu kuhusu Ebola.
Katika zoezi hilo ambalo Yanga watazunguuka katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa siku tano watatoa bure jumla ya tiketi za 10,000 kwa Mashabiki wao wataoshiriki kupata elimu na kuchanja.
Taarifa hizo zimetolewa leo na CEO wa Yanga SC Andrew Mtine pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Jackson Group Kelvin Twissa ambao ni Washirika wa Yanga SC upande wa masoko.