Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura ametangaza kuwa baadhi ya viwanja vimefungiwa kuchezewa michezo ya Ligi Kuu kutokana na kuharibika na kwa wale au timu zitakazopenda kuendelea kutumia viwanja hivyo basi wafanye marekebisho.
“Kamati imezuia baadhi ya viwanja vya mechi za Ligi Kuu kwa masharti kwamba wanaohusika moja wavifanyie marekebisho katika kipindi hiki ambacho Ligi imepisha mechi za kirafiki za kalenda za FIFA, au watafute viwanja mbadala wote wanaohusika tumeshawaandikia rasmi”>>>Boniface Wambura
VIDEO: Goli lililoipa Tanzania Ubingwa wa CECAFA U-20 dhidi ya Kenya