Labda tunaweza kudhani ni Tanzania tu ndio imeingia kwenye headlines za kufungia video za nyimbo kadhaa za Wasanii ila ukweli ni kwamba hata kwenye nchi zinazoizunguka Tz kama Uganda, Rwanda na Kenya zimefanya hivyo.
Post hii ni maalum kwa ajili ya stori kutoka Rwanda kuhusu video hizi tatu ambazo haziruhusiwi kuchezwa kwenye vituo vya TV kwa sababu zimevunja maadili ambapo Wizara ya Utamaduni iliitisha mkutano na Waandishi wa habari na kusema iko tayari kulipia gharama za video kurudiwa lakini ziwe na maadili, yani bila picha za uchi au za kimahaba zinazoonekana.
Rafiki yangu TK ambae ni mtangazaji wa TV Rwanda ananiambia Rais Paul Kagame alishawahi kusema kwenye moja ya hotuba zake kwamba pamoja na nyimbo kufungiwa, >>> ‘kufungia nyimbo za Wasanii kisa wamekiuka maadili sio dawa, tatizo ni walifundishwa maadili wakakiuka? kuwafungia sio dawa ya kuwafundisha utamaduni… kuna njia nyingine za kuwasaidia’
Hii ya kwanza hapa chini ni ya Urban boyz inaitwa ‘ancilla’
[youtube youtubeurl=”ekEMO-8Ifvk” ][/youtube]
Hii ya pili hapa chini ni ya msanii wa Rwanda ambae kamshirikisha Lamyia Good wa Marekani ambae aliwahi kufanya kolabo na Ay na Romeo Miller ‘speak with your body’
[youtube youtubeurl=”tzGT6QoL-pc” ][/youtube]
Hii ya chini ndio ilifanywa Tanzania inaitwa ‘uniguse’ ya Shanel
[youtube youtubeurl=”3tZR32wrzfA” ][/youtube]
Hii ya nne inaitwa arankurura ya Riderman ft Neg G General
[youtube youtubeurl=”JicmKn2qF_I” ][/youtube]
Ya tano ni hii ya Iri Joro – Christopher ft Danny
[youtube youtubeurl=”jc4X1WS6O5E” ][/youtube]
Baada ya kuzitama kuna kipi cha moyoni ulichonacho? zimesimamishwa kihalali?
Kama hutaki stori kama hizi zikupite, kazi yangu ni kuhakikisha zinakufikia kila wakati iwe usiku au mchana nakuwekea link kwenye twitter facebook na instagram kwa jina hilohilo la MillardAyo.