Nilichelewa kufahamu kwamba kumbe mastaa wa dunia kama kina Rihanna wanapotokea kupiga picha kwa ajili ya majarida mbalimbali duniani hulipwa pesa tena pesa nyingi kwa sababu ya hiyo kazi.
Hizi ni picha zilizopigwa Hollywood Hills Marekani kwa ajili ya magazine moja ya Ufaransa ambapo RiRi aliicha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.
Najaribu kufikiria ni kiasi gani cha pesa Jarida hulazimika kumlipa mtu kama Rihanna ili akubali kupigwa picha kama hizi?
Ni miongoni mwa mastaa wa kike wenye nguvu duniani ambapo mwaka 2013 alishika nafasi ya 17 kati ya Wasanii 20 waliolipwa pesa nyingi sana kwenye muziki wanaoufanya huku nafasi ya 10 ikishikwa na Beyonce, Justin Bieber alichukua nafasi ya 7, nafasi ya kwanza inashikwa na Madonna huku ya pili ikichukuliwa na Lady Gaga.