Stori Pekee

Hii kali, imetokea kweli wakati huyu mama akihojiwa na TV, mwizi akapita nae

on

Screen Shot 2014-04-11 at 2.33.38 PMMitaa mbalimbali nchini Brazil imekua ikitajwa kwa uhalifu kutendeka mara kwa mara hata wakati wa mchana lakini pia vilevile wizi huo umekua ukifanyika hata kwenye maeneo ambayo mgeni yeyote anaweza kuamini ni maeneo salama kutokana na ustaarabu unaoonekana lakini pia wingi wa watu.

Hii video hapa chini ni ya mama aliekua akihojiwa kwenye TV lakini ghafla akatokea mwizi na kutaka kupita na mkufu wake wa gold, mkufu huo haukua rahisi kunyofoka hivyo mwizi akakimbia na mikono yake mitupu.

Yani wezi kuibia watu ovyoovyo tu town imekua ni kitu cha kawaida kabisa kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini.

[youtube youtubeurl=”cr3j_1yjydo” ][/youtube]

Screen Shot 2014-04-11 at 2.42.38 PMHili ni onyo kwa mashabiki watakaokwenda Brazil kwa ajili ya kushuhudia mechi za kombe la dunia, unaambiwa mwezi uliopita Polisi wa Brazil wapatao 1400 wakiwa na magari maalum pamoja na msaada wa helikopta walivamia na kusafisha moja ya sehemu zinazoaminika kuwa na wezi wengi.

Unapenda stori kama hizi zisikupite? jiunge kwenye familia ya millardayo.com kupitia twitter facebook na instagram kwa jina la MillardAyo ili niwe nakutumia kila ninapozipata iwe usiku au mchana.

Tupia Comments