Michezo

Kama ilikupita, Azam FC ilivyochukua ubingwa.

on

Screen Shot 2014-04-14 at 1.41.56 AMMwandishi wa habari za michezo Saleh Ally ameanza kwa kuandika >> yametimia! hakuna kelele tena na Azam FC imefanikiwa kuweka rekodi mpya kwa kutwaa ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya kwanza ambapo iliukosa ubingwa huo mara mbili mfululizo ikishika nafasi ya pili.

Time hii Azam wamemaliza kazi kwa kuifunga Mbeya City 2-1 kwao Sokoine huku Azam ikitaka pointi tatu kumaliza kazi ambapo wageni ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Gaudence Mwaikimba katika dakika ya 45.

Mbeya City wakasawazisha kupitia Mwagane Yeya katika dakika ya 70 kabla ya nahodha John Bocco kutupia bao la pili na kuhitimisha safari yao ya kutwaa ubingwa wakiwa na mchezo mkononi dhidi ya Ruvu JKT.

kupitia salehjembe.blogspot.com Saleh anasema hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kutwaa ubingwa wa ligi luu bara huku ikipangua ‘minguvu’ ya wakongwe Yanga na Simba ambao wanabaki katika nafasi ya pili na nne.

Tupia Comments