Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amewataka vijana kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya umbea badala yake wachangamkie fursa za kiujasiriamali.
Meya Sitta ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mfumo maalum wa kuwasaidia vijana kujiajiri kupitia mitandao.
Amesema kuna watu wanapenda elimu ya ujasiriamali ila hawana muda wala uwezo wa kusafiri kupata elimu.
“Kupitia mfumo huu unaweza kujisomea kupitia simu yako ya mkononi ambapo kuna Application utaichota ambapo kuna course mwalimu atakufundisha,” -Sitta
Amesema kuwa ajira ni chache na waombaji ni wengi, hivyo vijana waende katika mitandao waongeze elimu.
“Vijana waombe mikopo lakini hawaombi, wanalalamika vijuheni wanaingia katika social media wanaangalia umbea tu, hivyo waje wajifunze ujasiriamali,” Sitta
LIVE MAGAZETI: Bajeti ya Uchaguzi, Mbowe afunguka, Baba Matatani kumbaka mwanae