Bomu la kienyeji lililolipuka ‘Arusha night park’ April 13 2014 Mianzini Arusha na kujeruhi watu 17 waliopelekwa kwenye hospitali tatu tofauti limefanya dau lililotolewa na Polisi liwe kubwa zaidi kwa yeyote atakaefichua muhusika wa huu mtandao wa mabomu Arusha.
Kamishna wa makosa ya jinai (DCI) Isaya Mghulu amesema watatoa shilingi milioni 10 kwa huyo atakaefanya kweli kwenye kufanikisha Walipuaji mabomu hao kujulikana na kukamatwa.
Kwenye sentensi nyingine, ameweka wazi kwamba mpaka sasa bado hata wale waliohusika na ulipuaji wa mabomu kwenye kanisa kule Olasiti na kwenye mkutano wa CHADEMA hawajakamatwa wala kujulikana lakini jitihada za kuwatafuta zinaendelea.
Pata kila kinachonifikia iwe usiku au mchana, nitakutumia kwenye twitter instagram na facebook @millardayo