AyoTV

Dr Tulia alivyoshiriki kuzikusanya Milioni 40 Mbeya

on

March 5, 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi katika matembezi maalum yaliyoambatana na harambee ya uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kusaidia watu wasiojiweza iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa CCM mkoani Mbeya ambapo zaidi ya Milioni 40 na laki tatu zilipatikana ikiwemo ahadi kwa kushirikiana na Mbunge wa viti maalum mkoani humo Dr Marry Mwanjelwa pamoja na wadau wengine akiwemo Mdau wa elimu Ndele Mwaselela.

Katika harambee hiyo Dr Tulia alichangia zaidi ya shilingi Milioni saba, Dr Marry Mwanjelwa Milioni tatu, Ndele Mwaselela Milioni 16 pamoja na kuwasomesha watoto 30 wasiojiweza.

Maamuzi ameyachukua Naibu Waziri wa Elimu kwa Mwalimu Mkuu

Soma na hizi

Tupia Comments