1. Kuanzia April 29 2014 Mwanaume na Mwanamke ambao wapo kwenye ndoa wana haki na majukumu sawa kwenye ndoa yao huko Kenya hii ikiwa ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini muswada wa ndoa na kuufanya kuwa sheria.
- Wengi wanadhani sheria hiyo sasa inaruhusu kila Mwanaume wa Kenya kuoa Mke zaidi ya mmoja lakini ukweli ni kwamba Wake wengi wanakubaliwa tu kwenye ndoa za Kiislamu na zile za Kiutamaduni.
-
Maamuzi ya Rais Uhuru Kenyatta ni tamati ya kazi aliyoianzisha baba yake ambae ni mzee Jomo Kenyatta mwaka 1967 ambapo kwa saini hii, sheria saba ambazo Wakenya wamekua wakitumia kutafsiri maswala ya ndoa zimejumuishwa chini ya sheria moja.
-
Sheria ya ndoa inaratibu aina tano za ndoa ambapo ukijiingiza kwenye moja wapo huwezi kujiingiza kwenye nyingine wakati upo kwenye ndoa hiyo na ndoa ambazo zinaruhusu mke mmoja tu ni za Kikristo pia zile za Kihindi.
5. Kama upo kwenye ndoa inayoruhusu mke mmoja peke yake alafu ukao mke wa pili kisheria unaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani na kwa wale wanaotaka kuoa zaidi ya mke mmoja inabidi wawe kwenye ndoa za Kitamaduni ambapo wanaruhusiwa wake wengi kwa kuzingatia mila na desturi zao.
- Wabunge walitupilia mbali mapendekezo ya awali kwamba idhini ya mke wa kwanza inahitajika pale Mwanaume anapotaka kuongeza mke wa pili ambapo mmoja wa Wabunge niliowasikia amesema haitakiwi mke mkubwa kuambiwa kuna mke mwingine anakuja, inabidi uje nae tu alafu ndio agundue hiki ni chuma kipya.
Kwa sasa kisheria hairuhusiwi kuoa mtoto ambae hajatimiza miaka 18 kama ilivyokua awali kwenye ndoa za kitamaduni.
Ndoa zote lazima zisajiliwe kwenye ofisi ya msajili wa ndoa.
Jiunge na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina la @millardayo niwe nakutumia stori kama hizi usiku na mchana baada tu ya kunifikia, kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi mtu wangu