Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abass leo August 1, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari Dar es Salaam kuzungumza mambo mbalimbali ambayo Serikali imekuwa ikiyafanya ikiwemo takwimu mbalimbali zinazoonesha ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Dr. Hassan amesema licha ya hali ya uchumi wa dunia kupita kwenye changamoto mbalimbali ikiwemo bei ya mafuta na hali ya chakula, lakini uchumi wa Tanzania unazidi kukua.
>>>”Tanzania inatajwa kuwa imara kwani ipo katika asilimia 7 ya ukuaji na katika eneo la Afrika Mashariki ni namba moja ikifuatiwa na Kenya ambayo ni asilimia 6. Pia nchi yetu ipo katika mageuzi hasa kwenye ukusanyaji wa mapato ambapo mwaka jana tulikuwa chini ya Trilioni Moja lakini kwa sasa imepanda.” – Dr. Hassan Abbas.
ULIPITWA? Waziri Makamba kuhusu Mpango wa Serikali kupunguza matumizi ya Mkaa na Kuni!!!