Baada ya kuwepo kwa video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadaiwa kuonesha namna mchele wa plastic unavyotengenezwa ikidaiwa pia kuwa mchele huo umekuwa unatumika na Watanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania ‘TFDA’ imetoa ufafanuzi kuhusiana na tukio hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Hiiti Sillo amekutana na Waandishi wa Habari na kutoa ufafanuzi juu ya madai hayo akianza kwa kukiri kuwepo kwa video hiyo nao wakatoa taarifa kwa Umma.
>>>”Nianze kwa kusema kwamba tarehe 8 mwezi Juni tulitoa taarifa ya ufafanuzi kwa Umma kuhusu taarifa iliyokuwa inasambaa ya video clip kupitia mitandao ya kijamii hasa mtandao maarufu ambao unaitwa WhatsApp kuhusu mchele ambao wanadai unatokana na plastic ambao upo kwenye soko na ambao unaweza kuwa na athari kwa watumiaji.
“Wamekuwa wakihusisha na mchele ambao unaitwa sunrice ambao ni brand moja wapo ya mchele wa Basmati. Tutoe ufafanuzi kwamba TFDA imesajili mchele wa Basmati lakini sio huo wa brand ya sunrice ambao taarifa zake zimekuwa zikisambaa kwamba hatuutambui na kwamba taarifa ile sisi tulipoipokea tukaanza kufanya ukaguzi wa ufuatiliaji na kiuchunguzi.” – Hiiti Sillo.
Aidha, Sillo amesema kuwa wametoa agizo kwa wakaguzi na wafuatiliaji waliopo kwenye ofisi za TFDA kuendelea kufuatilia chanzo cha taarifa hizo huku akikiri kwamba hadi kufikia asubuhi leo June 19, 2017 hakuna taarifa zozote zilizoripotiwa kuhusu mchele huo wa plastic.
“Tumeendelea kuwaagiza wakaguzi wetu kupitia Ofisi za Kanda za TFDA kama mnavyofahamu tunazo Ofisi za Saba za Kanda katika mikoa mbalimbali ya nchi yetu kwa ajili ya kufanya ukaguzi na udhibiti katika maeneo yale kwamba wanapofanya ukaguzi waelekeze nguvu katika kufanya ukaguzi kutafuta vyanzo vya taarifa hiyo kuhusu mchele unaosemwa wa plastic.
“Hadi kufikia taarifa nilizozipokea leo asubuhi kwa kweli hakuna mahali popote ambapo tumethibitisha tumepata taarifa kwamba huo upo kwenye soko letu.” – Hiiti Sillo
ULIPITWA? Baada ya tukio la Polisi kuwatawanya ka mabomu walemavu waliokuwa wameandamana na kufunga Barabara tukio hilo limewagusa wengi hasa Vyama vya Siasa. Huu hapa ni msimamo wa ACT Wazalendo baada ya Walemavu hao kupigwa mabomu DSM. Bonyeza PLAY kutazama!!!