Baada ya mapumziko ya mechi za kirafiki zilizokuwa katika kalenda ya FIFA kumalizika, Jumamosi ya April 1 2017 Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kwa Dar es Salaam Young Africans kuikaribisha Azam FC katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Vodacom.
Yanga ambao waliingia uwanjani wakiwakosa wachezaji wao kadhaa wa kikosi cha kwanza kama Donald Ngoma, Kamusoko na Amissi Tambwe, waliingia uwanjani na kufanikiwa kuifunga Azam FC kwa goli 1-0 goli ambalo lilifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 70 baada ya Aishi Manula na beki wake kushindwa kufanya mawasiliano.
Ushindi wa Yanga dhidi ya Azam FC katika Ligi Kuu unakuja baada ya miaka mitatu pasipo kupata ushindi, Yanga walikuwa hawajaifunga Azam FC toka mwaka 2014 wakiwa wamecheza michezo sita na kutoa sare michezo mitano na kupoteza mchezo mmoja Mei 6 2015 Yanga walipoteza kwa goli 2-1.
Ushindi wa Yanga 1-0 Azam FC leo umeiweka kileleni kwa kuizidi Simba kwa point moja na mchezo mmoja #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/1vBwt2WuVe
— millard ayo (@millardayo) April 1, 2017
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0