Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Anthony Joshua ameomba kujiuliza kwa Andy Ruiz

on

Baada ya bondia wa England Anthony Joshua kupoteza pambano lake la kwanza katika boxing, kwa kupigwa na bondia kutokea Marekani mwenye asili ya Mexico Andy Ruiz, Anthony Joshua amekubali kurudiana na bondia Andy Ruiz ili kujiuliza alikosea wapi.

Promota maarufu anayemsimamia Anthony Joshua kuandaa mapambano mbalimbali Eddie Hearn ametangaza kuwa Anthony Joshua atarudiana tena na Andy Ruiz katika kipindi cha mwezi November  au December kwani kipengele cha mkataba wao kinawaruhusu kurudiana kama mmoja wao atahitaji.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri June 1 2019 ndio lilichezwa pambano kati ya Athony Joshua dhidi ya Andy Ruiz na Anthony Joshua kupoteza kwa kupigwa Technical Knock Out (TKO) round ya 7, hivyo kuvunja rekodi yake ya kutopigwa katika mapambano yake 22 aliyokuwa kacheza awali huku akishinda kwa point moja na mengine yote TKO.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments