Michezo

VIDEO: Magoli ya Zlatan Ibrahimovic yaliyoipa Man United point tatu dhidi ya Southampton

on

Usiku wa August 19 ilikuwa ni siku ambayo mashetani wa jiji la Manchester klabu ya Man United waliwakaribisha Southampton katika dimba lao la Old Trafford kucheza mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu England baada ya mchezo wao wa awali kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya AFC Bournemouth ugenini.

Mchezo dhidi ya Sothampton ulikuwa ni mchezo ambao ulitarajiwa kuangaliwa na mashabiki wengi zaidi duniani kutokana na kuwa hiyo ndio ilikuwa mechi ya kwanza ya Paul Pogba aliyevunja rekodi ya usajili ya dunia akitokea Juventus ya Italia na kurejea Man United kwa pound zaidi ya milioni 100 baada ya kuondoka 2012.

3407

Katika mchezo huo staa mwenye kujiamini zaidi kama ilivyo kwa kocha wake Zlatan Ibrahimovic, alifanikiwa kupachika magoli mawili yaliyoipa Man United point tatu na kufikisha jumla ya point sita katika msimamo wa EPL, Zlatan alianza kupachika goli la kwanza dakika ya 36 kisha akahitimisha kwa kufunga goli la pili dakika ya 52 kwa mkwaju wa penati.

https://youtu.be/UoaO9roxzlY

ALL GOALS &PENALTIES : Azam FC vs Yanga August 16 2016, Full Time 2-2 penalties 4-1 

Soma na hizi

Tupia Comments