Top Stories

Wafanyabiashara waliohukumiwa kifungo cha miaka minne leo

on

Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo August 3, 2017 imewahukumu kifungo cha miaka minne wafantabiashara na wakazi wawili wa Dar es Salaam Athumani Rajabu Mussa na Zamuna Salimu baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa mali yenye thamani ya Tsh. Milioni 12.8.

Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi, Adelf Sachore baada ya kujiridhisha na hoja zilizotolewa na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi wanne.

>>>”Ninawahukumu kwenda jela miaka minne kila mmoja ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizi za wizi, ambao wamekuwa wakishindwa kuwa waaminifu.” – Hakimu Sachore.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, wakiwasilisha utetezi wao juu ya sababu ya kutopewa adhabu kali watuhumiwa hao waliiomba Mahakama kuwapa kifungo cha nje huku mshtakiwa wa pili akidai kuwa ana familia inayomtegemea utetezi ambao hata hivyo ulitupiliwa mbali na Mahakama hiyo.

Awali kesi hiyo ilikuwa na washtakiwa sita ambapo wanne kati yao Mahakama kuwaona hawana hatia.

KING MAJUTO KAFUNGUKA: “Nimezushiwa kifo mara 5, lazima nife lakini…” Play kwenye video hii!!

Soma na hizi

Tupia Comments