Pamoja na kuwa David De Gea ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Man United kwa misimu minne kati ya mitano aliyokuwa anaitumikia club hiyo, hivi karibuni amekuwa na wakati mgumu na wakati mwingine amekuwa akiruhusu kufungwa magoli ambayo yandaiwa kuwa ni mepesi sana kwa golikipa wa kiwango chake kufungwa.
Makosa ya uwanjani ya David Ge Gea yameigharimu Chelsea msimu huu lakini kosa lake lilitokea katika mchezo wa Jumapili ya April 28 2019 dhidi ya Chelsea katika sare ya 1-1 limekuwa gumzo, baada ya kufungwa goli na Marcos Alonso baada ya Antonio Rudiger kupiga shuti lililoshindikana kudakwa na De Gea na kujikuta Alonso akimalizia.
Kutokana na De Gea mwenye umri 28 kusuasua golini, sasa inaripotiwa kuwa Man United wanapanga kurudi Atletico Madrid kupiga hodi tena wakimtaka Jan Oblak aje kulinda lango la Man United, De Gea alijiuga na Man United 2011 akitokea club ya Atletico Madrid ya kwao Hispania, hivyo kuhitajika kwa Oblak kunatajwa kuwa kutampa changamoto De Gea ya kufanya vizuri.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23