Niliwahi kuuliza kwa mtu aliyewahi kufanya kazi kwenye vituo vikubwa vya TV Afrika kama MTV Base na Channel O akaniambia kila kitu huwa kinapangwa, yani nyimbo zinazochezwa zinapata nafasi kwa time maalum kutokana na ubora wake wa video na wimbo wenyewe.
Aliniambia kuna zile video huwa zinachezwa usiku sana na inakua mara moja kwa siku, hizo zinakua zimetii masharti yanayotakiwa lakini hazikufikia kwenye kilele kinachotakiwa ndio maana zitapata nafasi ya kuchezwa mara mojamoja lakini zile nyingine kali ndio utakuta zinachezwa hata mara tatu kwa siku, asubuhi mchana na jioni.
Kwenye TV kama hizi za kimataifa wanazingatia sana kucheza nyimbo kwa time, kuna time huwa kwao zina thamani hata kucheza tangazo la biashara hapo ni bei kubwa sababu utafiti unaonyesha wakati huo ni watu wengi wanatazama TV mfano asubuhi, mchana na jioni hivyo hata wimbo ukichezwa hapo ni mauzo makubwa kwa msanii.
Hongera kwa Mtanzania Feza Kessy ambae amepata time ya kuchezwa kwenye Big Base Breakfast ya MTV BASE ambapo kwenye time hiyo pia ziliambatanishwa hits nyingine kama kolabo ya Snoop Dogg na Jason Derulo, Nicki Minaj na Sauti Sol ‘sura yako’
Moja ya vigezo vinavyotumiwa na TV hizi kubwa kupokea video za Wasanii ni video yako inatakiwa kuwa bora kiasi kwamba ya Nicki Minaj ikichezwa alafu ikafata yako kusionekane kuna utofauti wa ubora kupishana.