Saratani imeendelea kuwa tishio Tanzania na sasa unaambiwa saratani ambazo zilikuwa hazijawahi kujitokeza au kuonekana kipindi kilichopita, sasa ndio kama zimezaliwa na watu mbalimbali Tanzania wanakutwa nazo.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka taasisi ya Saratani Ocean road Julius Shija amekaa na millardayo.com na kusema takwimu zinaonyesha kuwepo kwa saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kuliko miaka iliyopita Tanzania.
Kwenye sentensi ya pili akasema >>> ‘Watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa kuhusisha mdomo, saratani ya mdomo ipo na nyingine zinasababishwa na zinaa’
Anasema kwenye kupokea wagonjwa wapya kila siku kwenye taasisi hiyo, Wagonjwa waliopata saratani hiyo mdomoni na kwenye njia ya juu ya hewa baada ya kujamiiana kwa njia ya mdomo wanaongezeka na sasa wanapokea Wagonjwa 500 mpaka 600 tofauti na kipindi cha miaka ya tisini mwishoni na miaka ya elfu mbili mwanzoni walipokua wakipokea Wagonjwa 200–300.
‘Kufanya mapenzi na kuhusisha mdomo kunaleta saratani kupitia mdomo na sehemu ya juu ya hewa, virusi hivi vikifika kwenye sehemu ya juu ya hewa na mdomoni na vikakuta kuna mchubuko au uwazi wowote vitaingia kwenye hizi chembechembe za fizi kwenye ulimi na kwenye njia ya juu ya hewa, vitapenya ndani na kuharibu zile chembechembe na zitaanza kukua na kusababisha saratani’
Kwa kumalizia anasema virusi hivi kikawaida vinakuwa kwenye sehemu za siri na vinasambaa kwa njia ya kujamiiana na vinasababisha baadhi ya saratani kwenye sehemu za siri kwa mfano saratani ya shingo ya uzazi kwa Wanawake.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook