Rapa Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA ameachia Video na wimbo wa Dume Suruali ambao umesababisha mijadala kutokana na aina ya uandishi wa mashairi yaliyomo kwenye wimbo huo kuwatetea wanaume ambao hawatoi (Hawahongi) pesa kwa wanawake.
Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe amesema Madume Suruali kwa maana aliyoiweka kwenye single yake ni aina ya wanaume ambao hawana hela “Broke Nig***” na aliamua kutumia neno hilo kwaajili ya kuvuta attention ya watu kitu ambacho amegundua mwanzo watu hakuelewa wimbo una maana ipi mpaka walipousikiliza.
MwanaFA amefanya mahojiano na show ya Clouds 360 inayorushwa na kituo cha Clouds TV na kueleza mambo mengi kuhusu wimbo wake mpya pamoja na video pia maisha ya muziki na elimu yake kwa ujumla. Unaweza kuitamaza hapa kwa ufupi na usisahau kutembelea Youtube Channel ya Clouds360 kuipata full interview.
AUDIO: Yapo hapa mambo 17 aliyoongea Ruge Mutahaba kuhusu Muziki wa Tanzania, kuhusishwa na Beef na wasanii. Bonyeza play