Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti taarifa za mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya Rapper XXXtentacion yaliyofanyika June 18,2018 Robert Allen ameiomba Mahakama kumpatia dhamana kwa lengo la kwenda kumuangalia mpenzi wake ambaye ni mjamzito kwa sasa.
Inasemekana kuwa mtuhumiwa huyo amemuomba jaji anayesimamia kesi hiyo, ampatie dhamana ili apate nafasi ya kuwa karibu na mpenzi wake ambaye ni mjamzito, mpaka pale kesi yake itakapoanza kusikilizwa na amedai kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuhusu kesi inayomkabili.
Robert Allen alikamatwa Georgia Marekani baada ya kuonekana kupitia camera za nje ya duka la baiskeli akiwa katika eneo ambalo mauaji ya Rapper XXXtentacion yalitokea.
Robert akiwa miongoni mwa watuhumiwa wanne amesisitiza kuwa endapo ataachiwa huru basi atajishughulisha na kazi yake iliyokuwa ikimuingizia kipato na kuendelea kumsaidia mama yake mzazi.
EXCLUSIVE: “Sijaonana na Lulu, Yupo kwenye maisha ya mtoto wangu nitaruhusu amlee”