The Female Rapper Cardi B ameamua kuwachana wale wote ambao wamekuwa wakimsema vibaya nyuma ya mgongo wake kuhusiana na ujauzito kuwa hawezi kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja yani muziki na kuwa mama wa familia.
Wakati akipokea tuzo ya Best New Artist katika tuzo za MTV VIDEO MUSIC AWARDS zilizofanyika usiku wa August 20,2018 Marekani aliongea maneno hayo mbele ya wasanii wenzake huku wengine wakimpigia makofi kutokana na ujasiri aliounyesha.
Huku wengine wakidai kuwa maneno hayo aliyoyaongea Cardi B ni dongo kwa Nicki Minaj kutokana na wao wawili kuonekana kuwa na bifu ingawa wawili hao hawajawahi kuweka hadharani kuwa wanautofauti.
https://youtu.be/yqFJ1wC-afA
DC Mjema ajibu tuhuma za CHADEMA, “Ilala kuna Simba jike’