Ipate hii kutoka kwa mzazi mwenzake na staa Chege Chigunda ambaye amewatolea povu wanawake ambao wamekuwa wakimjia juu na kumsema vibaya kuhusiana na Chege na hivyo amewataka wanawake hao wabadilike kwa kupendana na kuonyeshana ushirikiano.
Hii ni kutokana na tetesi kudai kuwa ujumbe huo kupitia ukurasa wa instagram wa Zahra umemlenga Chege ambaye anadaiwa kuwa amezaa na mwanamke mwingine ambaye aliwahi kumtumia message Zahra na kumtaarifu kuhusiana na ishu hiyo.
Zahra aliandika “Ifikie stage wanawake tubadilike, kwanini wanawake hatupendani lakini? Kipindi Chege yuko bachelor hakuna hata mtu alishawahi kwenda kwenye media or social network yoyote na kumzungumzi vibaya, leo amekuwa star kiasi gani hadi mtake kumuharibia CV yake jamani , kipindi hakai na mwanamke mlikuwa mnamuona muhuni sio handsome na maneno ya kashfa kwa kaka wa watu”
“Hakuna hata aliokubali kuacha mambo yake na kuamua kumzalia kila mtu alikuwa anamdharau kwa style yake, leo mimi nimeamua kuishi naye na kumzalia mnaanza vitu vya ajabu ili baadae muanze kusema wasanii sio wanaume mbona kaachana na mzazi mwenzie? Kwanini uwe mvivu na wakati unapenda kula? Jaribu kwenda shambani anza kulima, palilia mazao yako uje uvune mwenyewe sio ukute kimepikwa tu uanze kula”
“Nipumzishe na DM zenu mtoto wa watu , wewe mwanamke uanemfanyia ubaya leo mwanamke mwenzako kumbuka na wewe kesho utafanyiwa hivyo hivyo, tujaribu kupendana na kusapotiana jamani, hakuna alokamilika hapa duniani , unamsema leo sijui anawanawake wengi, je wewe kwa mtu wako upo peke yako? Nabaki pale pale wanawake tupendane , ndio kwanza mtoto ana miezi mitatu mmeanza hivi haya nikizaa wa pili si mtanirushia mabomu? JITATHMINI ,UTHAMINIKE”
Good News: MILIONI 600 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Waalimu wa Sayansi