Mchekeshaji Idris Sultan ameguswa na kile ambacho kinaendelea kwa msanii na Mbunge wa Kyayondo Mashariki nchini Uganda Bobi Wine hii ni baada ya msanii huyo kukamatwa kutokana na kile kinachodaiwa kuiponda serikali iliyopo chini ya Rais Yoweri Museven.
Kupitia ukurasa wa twitter wa Idris Sultan amesema kuwa mara nyingine anaona aibu kuwa Mwafrika kutokana na watu kukosa maadili na misingi ya kukosa ushirikiano wa kutetea anachofanyiwa msanii huyo na serikali ya Uganda, huku wengine wakisema kuwa alichofanyiwa Bobi Wine ni haki yake .
“Mara nyingine naona aibu kuwa Mwafrika, tunakosa maadili ya msingi kutoka na mwaka 1962 Mandela alifungwa jela kwa miaka 27 na Waafrika waliungana kuomba uhuru, dunia pia iliungana sio weupe wala weusi lakini kwa sasa Bobi Wine amefungwa wengine wanadiriki kusema alistahili , aibu yako”
“Niliumia sana siku Polisi walipotaka Mama atawanyike wakampiga”